Rwanda yadhamiria kuongeza pato la Utalii kupitia Mikutano
Kigali Convention Centre na Hoteli ya Radisson Blu-Kigali |
Kigali: Bodi ya taifa ya
Maendeleo nchini Rwanda (RDB), imejiwekea malengo ya kukusanya Dola za
Kimarekani ifikapo mwisho wa mwaka huu kutokana na utalii wa mikutano.
RDB imeelezea matumaini makubwa ya kufikia malengo yake hayo ya
ukusanyaji mapato kutokana na nyanja ya utalii kwa kuzingatia makusanyo ya
mwaka jana ya Dola za Kimarekani milioni 47.
Mkurugenzi mkuu wa RDB, Clare Akamanzi, ameliambia gazeti The
East African kwamba idara ya utalii wa mikutano itaingiza fedha zaidi kufuatia
miundombinu iliyokamilika katika kipindi cha mwaka jana ikitarajiwa kuchangia
upanuzi wake.
“Tunaamini tumefanya
vizuri, iwapo tulijiwekea malengo ya kukusanya Dola za Kimarekani milioni 47
mwaka jana, ambazo ni sawa na asilimia 10 ya mapato yote yaliyoingizwa kutokana
na shughuli za utalii, kwani tulikadiria kuingia Dola za Kimarekani milioni
440."
Akamanzi ameongeza kuwa kadiri kasi ya ongezeko la mikutano
inayoandaliwa nchini, takwimu zinaonyesha kwamba kiwango kitakuwa mara nyingi
zaidi katika miaka ya usoni; Rwanda inatakiwa kuanya chini juu ili kuwavutia
waandaaji wengi zaidi wa mikutano.
Katikia kipindi cha mwaka jana, Rwanda ikuwa mwenyeji wa
mikutano mikubwa ya kimataifa ipatayo 18, ikilinganishwa na 13 iliyofanyika
nchini Kenya, huku Uganda ikiwa mwenyeji wa mikutano 10 ya kiwango hicho.
Hoteli ya Marriot kati kati mwa jiji la Kigali |
Kwa mujibu wa Akamanzi, kuzidisha mara nyingi idadi ya mikutano,
ni sanjari ya sera ya Rwanda ya kuinua utalii ambao msingi wake mkubwa ni Sokwe
wa milima ya Volkano.
Mwaka 2014, Rwanda ilikuwa mwenyeji wa mikutano 80 chini ya
mwavuli wa shirika la uhamasishaji na kutangaza shughuli za utalii wa Mikutano Rwanda
Convention Bureau, (RCB).
Kabla ya mwisho wa mwaka huu, shughuli tofauti zinazohusiana na
mikutano na makongamano zipatazo 20 zimepangwa kufanyika nchini Rwanda, ukiwamo
wa Africa Travel Association World Tourism Congress; na Kwita Izina (kuwabatiza
majina watoto wa Sokwe); matukio yanayowavutia watalii wengi kuelekea mwisho wa
mwaka.
Kileleni mwa mataifa ya Kiafrika yaliyopokea mikutano mingi ni
Afrika kusini iliyokuwa mwenyeji wa mikutano 125; miongoni mwake 62 ikifanyika
kwenye mji wa mwambao wa Cape Town. Nafasi ya pili inashikiliwa na Morocco
iliyopokea mikutano 37, ambapo 19 kati ya hiyo ikifanyika katika jiji la Marrakesh.
Comments
Post a Comment