Rwanda: Waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC waelezea matumaini makubwa ya uchaguzi wa amani na uwazi
Sehemu ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC |
Waangalizi wa Uchaguzi kutoka jumuiya ya Afrika mashariki wameelezea
matumaini makubwa kwamba uchaguzi wa Rais nchini utakaofanyika mwezi ujao
utakuwa wa amani na uwazi na wenye kutoa mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali mapema Ijumaa hii, kiongozi wa
ujumbe huo, aliyewahi kuwa makamu wa Rais wa Kenya, mzee Arthur Moody Awori
amesema hawatarajii kushuhudia matukio yasiyokuwa ya kawaida kipindi cha
uchaguzi wa Rais. Ameongeza kwamba mategemeo yao ni kuona uchaguzi wa amani na
wa mfano kwa mataifa mengine ya jumuiya ya Afrika mashariki na hata nje ya bara
la Afrika, huku akitoa mfano wa nchi kama Marekani.
Kiongozi wa Waangalizi wa EAC, Mzee Moody Awori |
Kwenye mazungumzo na waangalizi hao, Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya
Uchaguzi, Prof Kalisa Mbanda amewachagiza waangalizi kwa ujumla katika uchaguzi
utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao kufanya kazi kwa uadilifu na kuandika
ripoti zenye kudhihirisha uhalisia wa zoezi zima.
Jumuiya ya Afrika mashariki imeutuma ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi
unaoundwa na watu 30 kufuatilia uchaguzi wa rais nchini. Ni ujumbe unaoundwa na
baadhi ya wabunge wa bunge la jumuiya ya Afrika mashariki, wawakilishi wa
Kamisheni ya jumuiya hiyo inayohusika na haki za binadamu, idara zinazohusika
na uchaguzi katika jumuiya hiyo, asasi za Kiraia, wawakilishi wa vijana na
watumishi kutoka sekretarieti ya jumuiya ya Afrika mashariki.
11 ni kutoka nchini Tanzanmia, wengine idadi kama hiyo wakitokea nchini
Uganda, huku wawili wakitokea Sudan kusini na watano ni raia wa Kenya.
End
Comments
Post a Comment