Rais Kagame aweka jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bugesera
Rais Paul Kagame akiweka jiwe la msingi katika mradi wa uwanja wa ndege wa Bugesera |
Rais wa Jamhuri, Paul Kagame ameweka jiwe na msingi
kwenye mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa kimataifa wa ndege wilayani
Bugesera.
Rais Kagame amesema wanayarwanda wengi wanasubiri kwa shauku
kukamilika kwa Uwanja huo utakaogharimu Dola za Kimarekani milioni 818 hadi
kukamilika kwake na kuwataka makandarasi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa
wakati.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bugesera unajengwa jimboni
mashariki umbari wa kilometa 30 kutoka jijini Kigali. Katika tukio la kuweka
jiwe la msingi katika mradi huo, Rais Kagame ameambatana na viongozi mbali
mbali akiwamo Mkurugenzio mtendaji wa Kampuni ya Mota Engil Africa, Emmanuel
Mota. Kampuni hiyo ya barani Afrika inamilikiwa na raia wa Ureno.
Kwa mujibu wa Rais Kagame, mradi huo ni miongoni mwa
miradi mikubwa inayotazamwa na wengi kama muhimili muhimu wa uchumi wa Rwanda
na kupanua wigo wa kibiashara baina ya mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki,
maziwa makuu na bara zima la Afrika.
Mradi wa uwanja wa ndege wa Bugesera utagharimu $818 |
Uongozi wa Mota Engil Afrika umemuahidi Rais wa Jamhuri
kufanya kazi kwa uadilifu na kukamilisha ujenzi kwa wakati. Uwanja wa wa ndege
wa Kimataifa wa Bugesera utakaokuwa na ukubwa kuzidi uwanja wa kimataifa wa
Kigali, utajengwa kwa awamu mbili, huku awamu ya kwanza ikitarajiwa kukamilika
ndani ya miezi 17 kuanzia sasa.
Uwanja huo wa kisasa utahusisha majengo yatakayotumiwa na
abiria pamoja na maofisa wa uwanja huo katika eneo lenye ukubwa wa mita za
mraba elfu 30, ofisi za ukaguzi wa nyaraka za wasafiri zipatazo 22 pamoja na
malango ya kuingilia na kutokea 10. Uwanja wa kimataifa wa Bugesera pia utakuwa
na madaraja/ngazi sita zitakazotumiwa na abiria kupanga ama kushuka ndani ya
ndege bila kulazimika kushuka chini kwenye njia ya ndege.
Comments
Post a Comment