Vibali vya ujenzi na ukarabati wa majengo vyaongoza kwa Rushwa-TIR
Ingabire Marie-Immaculee-Mwenyekiti wa TIR |
Shirika
linalopiga vita rushwa na uonevu (Transparency International) tawi la Rwanda
limeziorodhesha huduma za utoaji wa vibali vya ujenzi na ukarabati wa makazi
kileleni mwa huduma zinazoongoza kwa wahusika kutoa na kupokea rushwa.
Utafiti
wa Transparency International unaonyesha uwepo wa rushwa katika utoaji wa
vibali hivyo kwa kipimo cha asilimia 2.49 kwa asilimia 4.
Kati
ya idadi ya wananchi waliohojiwa na shirika hilo jijini Kigali na katika miji mingine
mikubwa nchini, asilimia 43.6 walionyehsa kuridhishwa na huduma wanazopatiwa
kwenye masuala ya ardhi, huku asilimia 39.8 wakidhihirisha kuridhika kiasi na
wengine zaidi ya asilimia 20 wakisema hawaridhiki na huduma wanazopatiwa na
maofisa wa masuala ya ardhi nchini.
Rwanda ni miongoni mwa Mataifa yanayodhihirisha kiwango cha chini cha rushwa |
Kwa
mujibu wa utafiti wa Transparency International, Wilaya ya Rusizi inaongoza kwa
kiwango kwa kipimo cha asilimia 18.4, huku Makatibu watendaji wa tarafa
wakitajwa kupokea rushwa ya hadi franga milioni moja.
Pia Maofisa usalama wa
tarafa na wilaya (DASSO) wanasemekana kupokea rushwa ya hadi franga laki saba.
Comments
Post a Comment