Waandamanaji wakibeba silaha za jadi eneo la Mathare (picha/Reuters) Huku asilimia zaidi ya 80 ya kura zilizopigwa yakiwa yametangazwa tayari nchini Kenya, Mgombea wa Muungano wa Upinzani (NASA), bwaba Rail Odinga amesema haafiki matokeo aliyoyaita ya "Uongo" huku akisema maofisa wa Muungano wa Jubilee wa Rais Uhuru Kenyatta wameingia kwenye mtandao na kubadili matokeo ili kumpatia ushindi mpinzani wake huyo anayewania muhula wa pili madarakani. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC), Uhuru anaongoza akiwa amefanikiwa kujikusanyia kura 7,984, 904 sawa na asilimia (54.3) wakati Odinga akipata kura 6,584,662 sawa na asilimia 44.8. Wafuasi wa Upinzani wakiandamana na kukabiliana na Polisi mjini Kisumu (Picha/Reuters) Punde baada ya Raila kutoa shutuma za wizi wa kura kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi eneo la Westlands, Waandamanaji wenye hasira walivamia mitaa ya Nairobi na mji wa Kusini magharibi wa
Popular posts from this blog
Uwanja wa Ndege Wa Kimataifa wa Kigali kileleni kwa safari nyingi za ndege Afrika mashariki
RwandAir imeongeza ndege kubwa zinazofanya ziara nje ya bara la Afrika Shirika la kimataifa linalohusika na safari za anga ForwardKeys, linabashiri kuongezeka kwa safari za ndege katika Uwanja wa kimataifa wa Kigali kabla ya mwisho wa mwaka huu ikilinganishwa na viwanja vingine maarufu vya ukanda wa Afrika mashariki. Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa ongezeko hilo litachangiwa na safari mpya za shirika la ndege la RwandAir kuelekea miji ya London na Bruxels barani Ulaya na Mumbai katika bara la Asia. Kwa mujibu wa ripoti ya ForwardKeys kufikia mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, safari za ndege katika ukanda wa Afrika mashariki ziliongezeka kwa asilimia 14.3% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Pia shirika hilo linesema kuwa viwanja vya ndege vya Afrika mashariki vinatumiwa kwa safari nyingi za ndani ya bara la Afrika ikilinganishwa na kanda nyingine za bara hilo, hali inayobashiriwa kuongezeka kuelekea mwisho wa mwaka huu. RwandAir inafanya safari katika
Serikali ya Tanzania yaipiga faini acacia Dola Bilioni 190
Kampuni ya Acacia inazalisha kiwango kikubwa cha fedha kutokana na Mgodi wa Bulyanhulu uliopo Dar Es Salaam (The East African): Serikali ya Tanzania imeipiga faini ya Dila za Kimarekani bilioni 190 ($190) kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia inayomiliki migodi tofauti nchini humo kama sehemu ya madai ya kodi, hali inayoweza kuongeza msuguano uliopo kuhusiana na kiwango cha mrabaha ambao serikali inasema kampuni hiyo inapaswa kuilipa. Kampuni hiyo imesema imepokea taarifa kuhusiana na kiwango hicho cha kodi mapema Jumatatu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kama limbikizo la madai ya kodi, yanayohusisha kipindi cha miaka 17 iliyopita. TRA inadai Acacia, ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji madini nchini Tanzania, inadaiwa na Serikali kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 154 ($154) kutokana na mgodi wa Bulyanhulu pamoja na kiasi kingine cha Dola za kimarekani bilioni 36 ($36) kutokana na Mgodi wa Buzwagi. Acacia inashutumiwa kusafirisha nje mchanga wen
Comments
Post a Comment