Posts

Uwanja wa Ndege Wa Kimataifa wa Kigali kileleni kwa safari nyingi za ndege Afrika mashariki

Image
RwandAir imeongeza ndege kubwa zinazofanya ziara nje ya bara la Afrika Shirika la kimataifa linalohusika na safari za anga ForwardKeys, linabashiri kuongezeka kwa safari za ndege katika Uwanja wa kimataifa wa Kigali kabla ya mwisho wa mwaka huu ikilinganishwa na viwanja vingine maarufu vya ukanda wa Afrika mashariki. Ripoti ya shirika hilo inasema kuwa ongezeko hilo litachangiwa na safari mpya za shirika la ndege la RwandAir kuelekea miji ya London na Bruxels barani Ulaya na Mumbai katika bara la Asia. Kwa mujibu wa ripoti ya ForwardKeys kufikia mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, safari za ndege katika ukanda wa Afrika mashariki ziliongezeka kwa asilimia 14.3% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Pia shirika hilo linesema kuwa viwanja vya ndege vya Afrika mashariki vinatumiwa kwa safari nyingi za ndani ya bara la Afrika ikilinganishwa na kanda nyingine za bara hilo, hali inayobashiriwa kuongezeka kuelekea mwisho wa mwaka huu. RwandAir inafanya safari katika

Polisi 140 wa Rwanda waelekea Haiti

Image
Polisi 140 wanaenda kuchukua mahali pa wenzao 160 wanaorudi nchini Juma hili Kundi la skari Polisi 140 wa Rwanda limeondoka nchini Jumatano jioni kuelekea kwenye ujumbe wa amani wa kimataifa nchini Haiti. Kundi hilo linalohusisha Polisi wa kike 20 linaunda awamu ya 8 ya Polisi maalumu wa kulinda amani (FPU VIII).   Hii ni awamu ya nane ya Polisi waliopewa mafunzo maalumu (FPU) kuelekea katika ujumbe wa amani wa Umoja wa mataifa nchini Haiti. Kundi hilo linaloongozwa na Kamishna msaidizi wa Polisi Yahya Kamunuga linaunda kikosi kijulikanacho kama RWAFPU-VIII  katika taifa hilo la visiwa vya Caribbean.    Katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali, Polisi hao 140 wameagwa na Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi, DIGP  Juvenal Marizamunda, aliyewatakiwa heri katika kutimiza majukumu yaliyopo mbele yao na kuwataka kuilinda hadhi ya Rwanda kimataifa. Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi ya Taifa, Kamishna msaidizi wa Polisi, Theos Badege askari polisi hao watakuwa na majukumu amb

Vibali vya ujenzi na ukarabati wa majengo vyaongoza kwa Rushwa-TIR

Image
Ingabire Marie-Immaculee-Mwenyekiti wa TIR Shirika linalopiga vita rushwa na uonevu (Transparency International) tawi la Rwanda limeziorodhesha huduma za utoaji wa vibali vya ujenzi na ukarabati wa makazi kileleni mwa huduma zinazoongoza kwa wahusika kutoa na kupokea rushwa.  Utafiti wa Transparency International unaonyesha uwepo wa rushwa katika utoaji wa vibali hivyo kwa kipimo cha asilimia 2.49 kwa asilimia 4. Kati ya idadi ya wananchi waliohojiwa na shirika hilo jijini Kigali na katika miji mingine mikubwa nchini, asilimia 43.6 walionyehsa kuridhishwa na huduma wanazopatiwa kwenye masuala ya ardhi, huku asilimia 39.8 wakidhihirisha kuridhika kiasi na wengine zaidi ya asilimia 20 wakisema hawaridhiki na huduma wanazopatiwa na maofisa wa masuala ya ardhi nchini. Rwanda ni miongoni mwa Mataifa yanayodhihirisha kiwango cha chini cha rushwa Kwa mujibu wa utafiti wa Transparency International, Wilaya ya Rusizi inaongoza kwa kiwango kwa kipimo cha asilimia 18.4,

Madrid watetea Kombe la Super Cup.

Image
Mabingwa wapya wa Super Cup 2017 Real Madrid  Klabu ya Real Madrid ambayo ni mabingwa wa Uhispania na Ligi ya mabingwa barani Ulaya (UCL) wametawazwa kwa mara nyingine kuwa mabingwa wa Kombe la Super Cup baada ya kuicharaza Manchester United mabao 2-1. Super Cup huzikutanisha timu zilizochukua makombe makubwa ya Ulaya, yaani Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho (Europa League). Casemiro aliifungia bao la kwanza Madrid  Mchezo huo uliochezwa kwenye joto kali la mji mkuu wa Macedonia Skopje, ulitawaliwa kwa sehemu kubwa na vijana wa Zinedine Zidane (Real Madrid), huku Manchester United inayofunzwa na Kocha wa zamani wa Real Madrid, Mreno Jose Mourinho wakifanya chini juu kuwabana mabingwa hao wa UEFA. Mabao ya Casemiro katika dakika ya 24 na Isco aliyepachika la pili dakika ya 54 yalitosha kuipatia taji la Super Cup Real Madrid, huku Mchezaji mpya wa Manchester United raia wa Ubelgiji akiifungia timu hiyo mabingwa wa Europa bao la kufutia machozi baada ya kupokea pasi muru
Image
Waandamanaji wakibeba silaha za jadi eneo la Mathare (picha/Reuters) Huku asilimia zaidi ya 80 ya kura zilizopigwa yakiwa yametangazwa tayari nchini Kenya, Mgombea wa Muungano wa Upinzani (NASA), bwaba Rail Odinga amesema haafiki matokeo aliyoyaita ya "Uongo" huku akisema maofisa wa Muungano wa Jubilee wa Rais Uhuru Kenyatta wameingia kwenye mtandao na kubadili matokeo ili kumpatia ushindi mpinzani wake huyo anayewania muhula wa pili madarakani. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC), Uhuru anaongoza akiwa amefanikiwa kujikusanyia kura 7,984, 904 sawa na asilimia (54.3) wakati Odinga akipata kura 6,584,662 sawa na asilimia 44.8. Wafuasi wa Upinzani wakiandamana na kukabiliana na Polisi mjini Kisumu (Picha/Reuters) Punde baada ya Raila kutoa shutuma za wizi wa kura kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi eneo la Westlands, Waandamanaji wenye hasira walivamia mitaa ya Nairobi na mji wa Kusini magharibi wa

Rais Kagame aweka jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bugesera

Image
Rais Paul Kagame akiweka jiwe la msingi katika mradi wa uwanja wa ndege wa Bugesera Rais wa Jamhuri, Paul Kagame ameweka jiwe na msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa kimataifa wa ndege wilayani Bugesera.  Rais Kagame amesema wanayarwanda wengi wanasubiri kwa shauku kukamilika kwa Uwanja huo utakaogharimu Dola za Kimarekani milioni 818 hadi kukamilika kwake na kuwataka makandarasi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bugesera unajengwa jimboni mashariki umbari wa kilometa 30 kutoka jijini Kigali. Katika tukio la kuweka jiwe la msingi katika mradi huo, Rais Kagame ameambatana na viongozi mbali mbali akiwamo Mkurugenzio mtendaji wa Kampuni ya Mota Engil Africa, Emmanuel Mota. Kampuni hiyo ya barani Afrika inamilikiwa na raia wa Ureno. Kwa mujibu wa Rais Kagame, mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotazamwa na wengi kama muhimili muhimu wa uchumi wa Rwanda na kupanua wigo wa kibiashara baina ya mataifa