Rwanda: Waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC waelezea matumaini makubwa ya uchaguzi wa amani na uwazi
Sehemu ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC Waangalizi wa Uchaguzi kutoka jumuiya ya Afrika mashariki wameelezea matumaini makubwa kwamba uchaguzi wa Rais nchini utakaofanyika mwezi ujao utakuwa wa amani na uwazi na wenye kutoa mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali mapema Ijumaa hii, kiongozi wa ujumbe huo, aliyewahi kuwa makamu wa Rais wa Kenya, mzee Arthur Moody Awori amesema hawatarajii kushuhudia matukio yasiyokuwa ya kawaida kipindi cha uchaguzi wa Rais. Ameongeza kwamba mategemeo yao ni kuona uchaguzi wa amani na wa mfano kwa mataifa mengine ya jumuiya ya Afrika mashariki na hata nje ya bara la Afrika, huku akitoa mfano wa nchi kama Marekani. Kiongozi wa Waangalizi wa EAC, Mzee Moody Awori Kwenye mazungumzo na waangalizi hao, Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi, Prof Kalisa Mbanda amewachagiza waangalizi kwa ujumla katika uchaguzi utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao kufanya kazi kwa uadilifu na kuandika ripoti z